24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mtoto wa Raila Odinga afariki dunia

Fidel-OdingaNAIROBI KENYA

MTOTO mkubwa wa kiume wa kiongozi wa upinzani wa Muungano wa Cord, Raila Odinga amefariki dunia jana asubuhi katika mazingira yasiyoeleweka.

Mtoto huyo, Fidel Odinga, alikutwa kitandani nyumbani kwake huko Windy Ridge, Karen baada ya kuutumia usiku wa jana na marafiki zake.

Mwili wa mfanyabiashara huyo, ambaye pia ni mwanasiasa kijana ulitarajiwa kupelekwa katika nyumba ya mazishi ya Lee Funeral Home.
Odinga, ambaye yuko eneo la tukio, alithibitisha kifo cha mwanae na kwamba alikula naye chakula cha mchana juzi Jumamosi kabla hajaenda kuungana na marafiki zake jioni ya siku hiyo.

Polisi walisema bado haijajulikani sababu ya kifo chake, na kwamba wanaendelea na uchunguzi.
Polisi wanasema uchunguzi wa awali unaonesha Fidel alikuwa na marafiki zake usiku wa Jumamosi na alirudi nyumbani mapema jana asubuhi.
Maofisa wa polisi kwa sasa wanachunguza mahali alipokuwa usiku huo na marafiki aliokuwa nao.

Kundi la wabunge na maseneta liliwasili nyumbani kwa Raila baada ya kupokea taarifa hizo za kusikitisha na kushtusha.

Viongozi mbalimbali wa kisiasa wameanza kutuma salamu za rambi rambi kwa familia ya Odinga.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles