28.6 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

MTOTO WA MIAKA MINNE ANAYEZUNGUMZA LUGHA SABA

MTOTO mwenye umri wa miaka minne amewashangaza wengi baada ya kuzungumza kwa lugha saba kwa ufasaha katika kipindi cha televisheni nchini Urusi.

Video inamwonesha msichana huyo,  Bella Devyatkina akionesha umahiri wake kwa sasa inavuta watu kote duniani baada ya msichana huyo kuzizungumza kiufasaha lugha hizo moja baada ya nyingine.

Msichana huyo mweye kipaji alishiriki katika kipindi hicho cha televisheni cha Urusi cha 'Udivitelniye Lyudi' yaani ‘Watu wa Ajabu’ akiwashangaza majaji mjini Moscow kwa ujuzi wake huo wa lugha.

Mbali ya kufahamu vyema Kirusi, Bella pia anazungumza Kiingereza, Kijerumani, Kihispania, Kifaransa, Kichina na Kiarabu kwa ufasaha; zote hizo ni lugha zinazotambulika rasmi kwa matumizi katika Umoja wa Mataifa.

Sehemu inayoshangaza zaidi ni kwamba Bella anaweza kuzungumza kwa ufasaha katika lugha hizo, huku ujuzi wake ukizidi ule wa msamiati wa mazungumzo rahisi ya kawaida.

Wakati wa kipindi aliweza kujibu maswali yaliyohusu mtaala wa shule kwa kutumia lugha hizo zote na hata kuimba nyimbo zao.

Mama wa Bella, Yulia anaeleza kuwa alianza kumfundisha bintiye huyo lugha hizo wakati alipokuwa na umri wa miaka miwili.

Walianza kwa somo la Kiingereza, lakini baadaye aliona kuwa Bella alikuwa akifurahia somo na hivyo akaanza kuongeza lugha nyingine za kumfundisha.

Bella alifanyia kazi lugha ya Kiingereza na mama yake huku lugha nyingine akifundishwa na wazungumzaji wa asili wa lugha hizo.

Kama ilivyotarajiwa wataalamu wa lugha wameshangazwa na uwezo wa Bella kama ilivyokuwa kwa watazamanaji walioshuhudia kwa macho, kupitia televisheni au kuiona video mtandaoni.

Mtaalamu mmoja wa lugha alikaririwa akisema: “kesi kama hizi ni nadra mno lakini zimewahi kutokea huko nyuma. Lugha hujikita katika ubongo wa mwanadamu na kuendelea katika hatua tofauti za maendeleo.”

Anaamini kuwa Bella hatapoteza ujuzi wake lakini alionya kwamba wakati fulani unaweza kupotea iwapo hautafanyiwa kazi mara kwa mara kimazoezi.

Wakati akiendelea kujifunza lugha, dogo Bella anasema ndoto yake ni kuwa nguva jike kama alivyo kipenzi chake Ariel wa picha ya vibonzo za Disney– ambaye pengine ni moja ya sababu ya Bella kuwa na uwezo wa kuzungumzia kiufasaha wanyama wa baharini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles