23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mtoto wa miaka 9 afariki kwa ebola Uganda

KASESE, UGANDA

MAOFISA nchini Uganda wamesema msichana wa miaka 9 kutoka  nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo aliyethibitishwa kuwa na virusi vya Ebola juzi Alhamisi amefariki nchini Uganda akipokea matibabu.

Kifo cha mtoto huyo ni cha tatu kutokea nchini Uganda ambapo Juni mwaka huu mtoto wa mdogo wa kiume alifariki dunia.

Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC limeandika kuwa mwanamume raia wa Uganda na mkewe wa Congo waliwapoteza watoto wao wawili wa kiume baada ya kurudi kutoka safari nchini Congo walikokwenda kuwaona jamaa zao.

Wakizungumzia kifo cha sasa, maofisa  wameeleza kuwa mtoto huyo alifariki wakati mazungumzo yakiendelea kuhusu kumrudisha Congo kwa matibabu.

Mama wa msichana huyo aliyewasili na mwanawe Uganda kupitia mpaka wa nchi hiyo na Congo wa Mponde – ametengwa na atarudishwa alikotoka kuangaliwa zaidi.

Mama na mtoto huo inaelezwa waliingia Uganda ambako walifika kutafuta matibabu.

Wizara ya afya Uganda ilithibitisha kisa hicho kipya cha ugonjwa wa ebola katika mji wa magharibi wa Kasese.

Msichana huyo alipatikana akiwa na homa wakati wa ukaguzi wa ebola katika eneo la mpaka wa Mpondwe.

Sampuli ya damu iliyotumwa kufanyiwa ukaguzi juzi  Alhamisi jioni imethibitisha kwamba mtoto huyo alikuwa na ebola.

Kabla mauti ya hajamkuta msichana huyo alitengwa na kuhamishwa katika kituo cha kuwashughulikia wagonjwa wa ebola.

Akizungumza na BBC jana, msemaji wa wizara ya afya nchini Uganda, Ainebyoona Emmanuel alisema kuwa;

 “Msichana huyo na mama yake waliingia nchini kupitia mpaka wa Mpondwe kutafuta matibabu katika wilaya ya Bwera Kasese … alitambuliwa katika eneo hilo la kuingilia na kikosi cha ukaguzi akiwa na dalilia zifuatazo; joto jingi, mwili kudhoofika, upele na damu inayovuja kutoka mdomoni,”.

Alisema alitengwa na kufikishwa katika kitengo cha hospitali ya Bwera  ambako utaratibu  ulikuwa unapangwa kwa ajili ya kumrudisha Congo ambako kuna matibabu mazuri zaidi

Uganda imeidhinisha na kuendeleza kwa ufanisi vituo vya ukaguzi katika mpaka wake na Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo katika jitiahada ya kuuzuia mlipuko uliosababihsa vifo vya karibu watu 2000 katika mwaka uliopita.

Dalili za awali  za ugonjwa huo ni pamoja na homa ya ghafla, kudhoofika haraka, maumivu ya misuli na kuumwana koo.

Kiwango kinapozidi mtu anaweza kuanza kutapika, kuharisha na mara nyingine – kuvuja damu ndani na nje ya mwili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles