23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MTOTO WA MIAKA 6 APATA HESHIMA YA KIPEKEE KUTOKA KWA OBAMA

boy_writes_letter_to_obama-large_transnjjoebt78qiaydkjdey4cngtjfjs74myhny6w3gnbo8

New York, Marekani

Mtoto Alex (6) wa New York, Marekani amepata heshima ya kipekee kutoka kwa Rais wa Marekani Barack Obama baada ya kujitolea kumchukua Omran Daqneesh kijana aliejeruhiwa na bomu nchini Syria.

Mtoto huyo ambaye ni raia wa Marekani, amepewa pia heshima na maelfu ya watu baada ya kuguswa na hali aliyokuwa nayo mtoto Omran, hivyo kuamua kumwandikia barua Rais Obama kumsihi wamsaidie.

Baada ya taarifa ya habari kurushwa kupitia luninga, Alex na wengineo waliiona sura ya mtoto wa miaka 5 akiwa amekaa kwenye gari ya kubebea wagonjwa huku ametapakaa vumbi na damu, iliushtua ulimwengu na kumhamasisha kijana Alex kutoka Scarsdale, New York kuchukua hatua.

Taarifa zinasema baada ya tukio hilo, Alex aliandika barua kwa mkono na kuituma Ikulu ya Marekani, Alex alimuomba Rais Obama kwenda kumchukua Omran Syria na kumleta nyumbani kwao (Marekani) ambapo yeye na familia yake watamhudumia kwa dhati.

Naye Alex alisema kuwa Omran atakuwa mmoja kati ya wana familia na atamfanya kaka yake. Pia atamfundisha kuongea kiingereza, kuendesha baiskeli na kuongeza kuwa atachezea pia midoli ya Catherine dada yake.

Zaidi ya hapo, Rais Obama alisoma maneno hayo ya Alex kwa sauti wakati akitoa hotuba kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wiki hii kabla ya kuiweka video ya Alex akisoma barua yake mwenyewe kwenye mtandao wa Facebook.

maxresdefault

Kwenye ujumbe wake, Obama aliwaomba watu wasome barua ile ili wajue ni kwanini ameamua kuishirikisha dunia.

“Haya ni maneno ya mtoto wa miaka 6, mtoto mdogo asiye na uoga kwa watu wengine sababu ya sehemu walikotokea, muonekano wao au jinsi wanavyosali,” aliandika Rais Obama.

“Wote tunatakiwa kuwa kama Alex, hebu fikiria dunia ingekuwaje kama wote tungekuwa hivyo,” aliongeza.

Muda ilipokua inaandikwa, stori hiyo ilikua tayari imeshapata zaidi ya ‘likes’ 100,000 na kusambazwa zaidi ya mara 60,000 huku watumiaji wengi wa mtandao wa Facebook wakisifia huruma iliyooneshwa na Alex.

Moja wa watumiaji wa mtandao wa Facebook aliandika, “Huyu ni mtoto wa miaka 6 alie na utu, upendo na uelewa zaidi ya watu wazima. Pongezi kwa wazazi wake na najua dunia itaona mambo mengi makubwa kutoka kwa Alex.” (Source: CNN)

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles