30.4 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

Mtoto wa miaka 17 mbaroni kwa tuhuma za kumuua baba yake

Na Ashura Kazinja-Morogoro

JESHI la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia mtoto wa miaka 17 kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, alidai kuwa Mei 31, saa 12 alfajiri Kitongoji cha Manyani, Kata ya Mkalama wilayani Gairo, mtu aliyejulikana kwa jina la Issaya Lameck (41), maarufu kama Kusaganika, fundi Muwashi, aliuawa kwa kupigwa na mtoto wake mwenye miaka 17 (jina linahifadhiwa kwa sababu za kimaadili).

Kamanda Mutafungwa alisema siku ya tukio hilo, Issaya alirudi nyumbani akiwa amelewa, ndipo ulipozuka ugomvi ambapo mtoto wake anadaiwa alimpiga ngumi sehemu za usoni na alipodondoka chini aliendelea kumkanyaga sehemu za tumboni hali iliyosababisha kupata maumivu makali.

Alisema baada ya tukio hilo, ndugu wa Kusaganika walioamulia ugomvi huo, hawakuweza kumpatia msaada wa kimatibabu kutokana na hali ya ulevi aliyokuwa nayo wakati wa tukio.

Kwamba pamoja na mwenyewe kudai hajaumia, lakini ilipofika saa 12 alizidiwa na kufariki dunia.

Kamanda Mutafungwa alisema mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na daktari na kwamba umekabidhiwa ndugu kwa taratibu za mazishi.

Katika tukio lingine lililotokea katika Kitongoji cha Kasiki wilayani Kilosa, Kamanda Mutafungwa alisema saa 1 asubuhi Juni 1, askari polisi kwa kushirikiana na askari wa wanyama pori wa Hifadhi ya Mikumi wakiwa doria na misako, walipokea taarifa za kuwepo kwa mtu mwenye nyara za Serikali.

Alieleza walipofuatilia walifanikiwa kumkamata Nuru Mohamed (35) mkulima mkazi wa Kasiki akiwa nyumbani kwake, na baada ya kufanya upekuzi ndani ya nyumba yake alikutwa akiwa na pembe ya ndovu yenye kilo 7.5, yenye thamani ya Sh 34,635,000 ikiwa imehifadhiwa kwenye mfuko wa salfeti kisha kufichwa chini ya uvungu wa kitanda.

Kamanda Mutafungwa alisema mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na kwamba hatua za kumfikisha mahakamani zitafuata.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,854FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles