24.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Mtoto wa Kanye West apagawisha Paris Fashion Week

Paris, Ufaransa

MTOTO wa rapa Kanye West, North West, juzi aliwaacha mashabiki midomo wazi baada ya kupanda jukwaani na kuimba mbele ya idadi kubwa ya watu.

North mwenye umri wa miaka sita alikuwa kwenye tamasha hilo la baba yake ambalo linajulikana kwa ajili ya Yeezy Paris Fashion Week.

Kupitia kurasa za mitandao ya kijamii mastaa mbalimbali walionesha kushangazwa na jinsi ya mtoto huyo wa Kanye alivyokuwa anajiamini mbele ya idadi kubwa ya mashabiki.

“Angalieni viatu vyangu ni vipya na vipo vizuri, naweza kutembea navyo mtaani, angalia shule yangu ni mpya, hii manaake ni nini? Aliimba North mbele ya mashabiki.

Mashabiki walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa, North ameonesha kuwa mtoto wa nyoka ni nyoka kwa kuwa baba yake ni mmoja kati ya marapa wakubwa duniani.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles