23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

Mtoto mwenye matatizo ya ukuaji aomba msaada

Mwandishi wetu

Mtoto mwenye umri wa miaka minne, Ahilati Selemani,  anahitaji msaada wa matibabu baada ya kushindwa kupitia hatua za ukuaji kutambaa na kukaa kama watoto wengine. 

Akizungumza mapema leo, mama mzazi wa mtoto huyo, Salma amesema matatizo ya mtoto huyo yalianza baada ya kuzaliwa na kukutwa na manjano.

“Baada ya kujifungua nilikaa siku tano na ndipo mtoto akakutwa na manjano alipopata ugonjwa huo tulilazwa hospitali ya Mwananyamara kwa kupata matibabu na baadae kuruhusiwa kurudi nyumbani”

Aidha anasema baada ya kurudi nyumbani ukuaji wa mtoto haukuwa wa kawaida kama walivyo watoto wengine hivyo wakampeleka hospital  ya Msasani.

“Msasani wakampima wakasema anatakiwa kufanya mazoezi ya viungo hasa mgongo ili aweze kukua kwa kupitia staji zote anazopitia mtoto wa kawaida”anasema

Aliongeza kuwa anawaomba watanzania wamsaidie mtoto wake aweze kupata vipimo na matibabu ili aweze kukuwa kama watoto wengine kwa kuwa ana umri wa miaka 4 na hakai wala atembei.

 Kwa yeyote anayetaka kumsaidia awasiliane nae kupitia 0716007640.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,642FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles