27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

‘MTOTO MMOJA KATI YA WATATU HUFANYIWA UKATILI’

NA CHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAM

SERIKALI imesema utafiti wa idadi ya watu na afya ya mwaka 2010, unaonesha mtoto mmoja kati ya watoto watatu wa kike walifanyiwa ukatili wa kingono.

Pia takwimu hizo zinaonesha kuwa mtoto mmoja kati ya watoto saba wa kiume walifanyiwa pia ukatili huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa uzinduzi wa vipindi maalum vya Radio Times 100.5 Fm kuhusu mpango kazi wa kitaifa wa kutokomeza ukatili, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga,  alisema takwimu hizo zinaonesha jinsi tatizo hilo lilivyo kubwa ndani ya jamii.

Sihaba alisema pia katika takwimu hizo zinaonesha watoto 15 kati ya 100 wa kike hapa nchini walifanyiwa ukeketaji na wengine wanawake wenye umri kati ya miaka 15- 49 walifanyiwa ukatili wa shambulio.

“Serikali inatambua kwamba kuendelea kuwepo kwa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kutadhoofisha dhamira ya kufikia maendeleo ya kitaifa tuliyojiwekea hivyo jitihada za wadau mbalimbali zinahitajika kutokomeza vitendo hivi,” alisema Sihaba.

Alisema ipo haja ya jamii kushirikiana kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa sababu madhara yake ni makubwa.

Sihaba alisema uzinduzi wa vipindi katika radio hiyo kutaleta chachu kwa jamii kufahamu kwa undani jinsi ya kuepuka na kutoa taarifa za matukio haya.

Alisema tatizo la ukatili dhidi ya wanawake linaathiri maendeleo ya kitaifa ambapo huwapunguzia wanawake na watoto uwezo wa kupata haki ya kushiriki shughuli mbalimbali za uzalishaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles