28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Mtoto miezi 10 apata corona Rwanda

KIGALI, RWANDA

WIZARA ya afya nchini Rwanda imetangaza kuwa watu wengine sita wameambukizwa virusi vya corona miongoni mwao akiwamo mtoto mchanga wa miezi 10.

Maambukizi hayo yanaifanya Rwanda kuwa na idadi ya visa 17 vya maambukizi ya virusi vya corona.

Walipatikana na maambukizi hayo wote walikua wametoka katika nchi za ng’ambo hivi karibuni.

Wizara ya afya imewataja watu hao sita kuwa ni:

Mwanamke Mfaransa mwenye umri wa miaka 30 na mtoto wake wa miezi 10. 

Mume wake mama huyo alikuwa pia amepatikana na virusi siku zilizopita.

Mtoto wa miezi 10 ndiye mtu mwenye umri mdogo zaidi aliyepatika kuwa na virusi vya corona nchini Rwanda tangu ilipogundulika nchini humo wiki iliyopita

Mwingine ni Mnyarwanda mwenye umri wa miaka 32 aliyefika nchini Rwanda akitokea Dubai Machi 19 mwaka huu

Wengine ni wanaume kutoka Sweden waliofika Rwanda  Machi 03,2020 lakini wakaonyesha dalili za virusi vya corona Machi 18,2020

Mwanaume Myarwanda mwenye umri wa miaka 32 ambaye amekua akifanya safari katika mataifa ya kigeni naye  alipatikana na dalili  Machi 18,2020

Na mwingine ni Mwanaume Mnyarwanda mwenye umri wa miaka 24 aliyefika Rwanda Machi 19,2020 akitokea nchini  India kupitia Doha – Qatar.

Kulingana na wizara ya afya nchini humo wagonjwa wote wametengwa na wanaendelea kupata matibabu.

Serikali ya Rwanda imewaomba watu wote waliofika nchini Rwanda katika kipindi cha siku 14 zilizopita kujitenga wao wenyewe  kwa siku 14 na kufuata maagizo yaliyotolewa juu ya virusi vya corona.

Waziri wa Afya nchini humo, Anastase Shyaka alitangaza kufungwa kwa shule zote za umma na za binafsi, maeneo ya kuabudu na sehemu zote za umma.

Matukio kama vile mikusanyiko ya watu katika maeneo ya michezo na harusini vimeahirishwa na wale waliopoteza wapendwa wao watazikwa kwa namna ya kipekee.

Shirikisho la Soka la Rwanda (FERWAFA), pia limetangaza kwamba michuano yote kwa sasa itafanyika bila kuhudhuriwa na mashabiki katika viwanja vya michezo, huku shirikisho la mpira wa mkono nchini humo likiahirisha michezo yake yote.

Kanisa la Mtakatifu Karoli Lwanga lililopo katika eneo la Nyamirambo mjini Kigali jana milango yake ilifungwa kutokana na hofu ya maambukizi ya virusi vya corona.

Maeneo ya umma na maeneo yote ya utoaji wa huduma yameagizwa kuweka vitakasa mikono kwa ajili ya watu wanaotembelea maeneo hayo.

Raia wamehimizwa kukaa nyumbani na kuepuka matembezi yasiyo ya maaana na kunawa mikono mara kwa mara kwa muda wa sekunde 20.

Hakuna abiria atakayeruhusiwa kusimama na kutoa wito kwa watu wa eneo na vikosi vya usalama kusaidia kuhakikisha hatua hizo zinatekelezwa.

Baadhi ya dalili za virusi vya corona ni kikohozi, kushindwa kupumua vema na uchovu.

ZIMBABWE YAWA YA 38 AFRIKA 

Zimbabwe imekuwa nchi ya nchi ya 38 barani Afrika kuthibitisha ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) baada ya mwanaume mwenye miaka 38 kuthibitika kuambukizwa.

Bara la Afika limerekodi takribani visa 1000 vya maambukizi ya virusi vya corona. 

Hadi sasa idadi ya vifo imefikia 17 barani humo. 

Kuna hofu kwamba mifumo duni ya afya ya kitaifa barani Afrika italemewa kwa haraka na mripuko wa virusi hivyo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles