Mtoto huyu anatafutwa na wazazi wake, amepotea Sikukuu ya Christmas

0
745

Mtoto Steven Mselle (17), mkazi wa Kimara Suca, anayesoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Mchikichini jijini Dar es Salaam anatafutwa na wazazi wake baada ya kupotea tangu Desemba 25, mwaka huu.

Baba mzazi wa mtoto huyo, Arnold Mselle amesema ameshamtafuta tangu siku hiyo bila mafanikio ambapo ameomba msaada wa Watanzania kumsaidia kumpata mtoto wake.

Amesema siku hiyo aliondoka nyumbani saa saba mchana ambapo aliaga anakwenda kunyoa na alikuwa amevaa fulana ya nyekundu ya Arsenal na suruali ya jinzi.

“Siku ya kwanza tumemtafuta tukahisi labda ametoroka kwenda kula sikukuu na rafiki zake lakini kesho yake tukasema hapana tukaanza kumtafuta bila mafanikio na Desemba 27 tukapata wasiwasi zaidi tukaenda kuripoti katika Kituo cha Polisi Temboni tukapewa KMT/RB/3448/2019/TAARIFA.

“Tumemtafuta hadi Muhimbili (Hospitali ya Taifa ya Muhimbili), Amana (Hospitali ya Amana) na vituo vya polisi vyote bila mafanikio,” amesema.

Aidha, Mselle ameomba yeyote atakayefanikisha kupatikana au kumuona mtoto huyo atoe taarifa kituo chochote cha polisi au apige namba 0783940158 /0715532994/0714361089.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here