30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 31, 2023

Contact us: [email protected]

MTOTO HUSAIDIA KUONDOA TOFAUTI ZA WAZAZI

NA AZIZA MASOUD,

WATU wanapoamua kuingia katika uhusiano na kuishi pamoja ama kufunga ndoa, kunakuwa na sababu mbalimbali ikiwemo upendo walionao baina yao.

 Pamoja na kusukumwa na upendo walionao, pia uhitaji mkubwa ni kuwa na familia.

Kuwa na familia iliyokamilika kunajumlisha kuwa na mke au mume pamoja na watoto.

Wanandoa wanapopata mtoto anakuwa kama moja ya kiungo kinachochangia kuwaunganisha katika mambo mengi.

Kutokana na sababu hizo, mtoto anatajwa kama kiungo muhimu katika familia hasa kwa wazazi.

Mara nyingi wanandoa ama wapenzi wanapokuwa na mtoto si rahisi kuwaona wanakuwa na ugomvi ambao unaishi muda mrefu kama inavyokuwa kwa watu wasio na watoto.

Wapo ambao wanakuwa na ugomvi wa mara kwa mara lakini mara nyingi huwa wanawahi kusuluhisha kupitia njia mbalimbali ili kufanya familia ikae sawa.

Wazazi wengi wanapokuwa katika migogoro hulazimika kuishi nyumba moja kwa makubaliano ama ya kulala vyumba ama vitanda tofauti.

Hii inachangiwa kuwaza mambo mengi  endapo watatengana ama kuachana kabisa kila mtu kuishi kivyake ikiwemo suala la ustawi wa mtoto.

Watoto wanaposhuhudia ugomvi wa  wazazi wao wanakuwa katika hali ya unyonge na wengine wanafikia hatua ya kushindwa kutekeleza majukumu yao ikiwemo yakimasomo.

Wapo wazazi ambao hawapendi kuona watoto wakisononeka kwa sababu ya ugomvi unaoendelea ndani ya nyumba.

Baadhi ya wazazi wanakuwa katika migogoro mikubwa na kufikia hatua ambayo haiwezi kusuluhishwa lakini  wanalazimika kuishi pamoja kwa sababu ya mtoto.

Mtoto anaposhuhudia wazazi wanagombana si sawa kwa sababu mara nyingi inamfanya asiwe katika hali nzuri, wapo wengine wanashindwa hata kuwa makini katika mambo yanayowahusu kama masomo.

Wazazi wenye busara wakishagundua hali hiyo kwa mtoto wao huamua kukaa chini na kusuluhisha.

Pia kuna ugomvi wa wazazi ambao hutatuliwa na watoto hasa wale wanaokuwa katika umri wa kujitambua.

Wapo watoto ambao hulazimika kuchukua jukumu la kuwasuluhisha wazazi ama kwa vitendo na wengine hufikia hatua ya kuwaweka vikao.

Haya yote yanaonyesha jinsi gani mtoto alivyo na nguvu kuhakikisha wazazi hawatengani ama kuachana kirahisi.

Wazazi mnapaswa kufikiria mara mbili mnapofikia uamuzi wa kuachana kwa kuwa mara nyingi katika uamuzi huo wanaoumia ni watoto kwa kiasi kikubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles