27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Mtoto aliyejeruhiwa na tembo akabidhiwa milioni 1.5

MWANDISHI WETU-ARUSHA

Kampuni ya Green Mills Safari Ltd inayondesha shughuli za utalii wa uwindaji wilayani Longido mkoani Arusha imekabidhi Sh milioni 1.5 za matibabu kwa mtoto Ngayeyo Olosiana aliyejeruhiwa na tembo.

Msaada huo ulikabidhiwa jana Ijumaa Julai 19, kwa Baba mzazi wa mtoto huyo, Ngulana Naiyo, katika hospitali ya Selian mjini Arusha alipolazwa.

Akikabidhi msaada huo wa mwakilishi wa Kampuni hiyo Amir Mvungi alisema Green Mills wametoa msaada huo kama sehemu ushirikiano wa jamii inayowazunguka.

“Tukio hili limetusikitisha, tumetoa kidogo ili kisaidia matibabu ya mtoto huyu aliyejeruhiwa na tembo, tutaendelea kushirikiana na wananchi kwa kadri tunavyoweza,” alisema Mvungi.

Naye baba wa mtoto Naiyo alishukuru kwa msaada wa fedha hizo akisema zitaisaidia familia yake kumtibu mtoto wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,404FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles