28.2 C
Dar es Salaam
Monday, February 6, 2023

Contact us: [email protected]

MTOTO ALIYEISHI KWA KULA MAFUTA ATAMANI KUWA DAKTARI BINGWA

 

 

Na VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

MTOTO Shukuru Kisonga (16) ambaye ameishi muda mrefu kwa kula sukari robo tatu, mafuta ya kula lita moja na maziwa lita tatu, amesema ndoto yake ni kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya damu.

Shukuru alisema hayo jana alipozungumza na MTANZANIA kuhusu maendeleo ya afya yake na kuongeza kuwa ataongeza juhudi katika masomo yake afikie ndoto yake hiyo.

"Niliteseka muda mrefu, namshukuru Mungu sasa sijambo naendelea na matibabu wodini, nikiruhusiwa kurejea nyumbani nitaongeza juhudi katika masomo yangu nitimize ndoto yangu ya kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya damu, " alisema.

Shukuru alisema anataka kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya damu   awasaidie watu wengi hasa wanaoteseka na ugonjwa kama unaomsumbua yeye.

" Namshukuru daktari wangu hapa Hospitali ya Taifa Muhimbili, amenisaidia mno ndiyo maana na mimi ninataka kuwa kama yeye   niweze kuwasaidia wengine wanaougua Mungu akinijalia, " alisema.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya damu, Stella Rwezaula, juzi alisema mtoto huyo anaugua selimundu, ugonjwa ambao amezaliwa nao baada ya kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi wake.
 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles