24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mtikila aipinga Mahakama ya Kadhi kortini

mtikilaNa Kulwa Mzee, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, amekimbilia Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupinga Mahakama ya Kadhi na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu kuwekwa kwenye Katiba ya nchi.

Mtikila, ambaye hakuwa na wakili wa kumwakilisha, aliifungua kesi hiyo ya kikatiba katika Masijala Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kupewa namba 14 ya mwaka huu.

Viongozi wa juu serikalini waliapa kwa ajili ya kuilinda Katiba, lakini wao wanavunja Katiba kwa kukubali kuwepo kwa mahakama hiyo na OIC, hivyo anaomba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, baadhi ya mawaziri na viongozi wengine wa juu serikalini waitwe mahakamani kujieleza kwanini wasifungwe jela miaka isiyopungua mitano kwa kuvunja katiba.

Katika hati yake ya madai, Mchungaji huyo aliwataja wanaotakiwa kuitwa kujieleza kwanini wasifungwe kuwa ni Waziri Pinda, Mary Nagu, Asha Rose Migiro, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, Stephen Wasira, Ernest Ndikilo, Karim Yunus, Issa Njiku, Danny Makanga na wengine.

Anadai Mahakama ya Kadhi haifai kabisa kuwepo nchini kwa sababu inakwenda kinyume cha haki za binadamu na haki nyingine za msingi, ikiwemo kuwanyima uhuru watu ambao si Waislamu nchini.

Mchungaji Mtikila anadai kwamba kwa mujibu wa kifungu namba 12 na 13 cha Katiba ya nchi, kinaeleza kwamba watu wote ni sawa kisheria, hakuna aliyekuwa juu ya sheria hivyo wanaovunja Katiba na sheria wanasababisha vurugu nchini.

Alitolea mfano waliofungwa kwa ajili ya kuvunja sheria, akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi BoT, Amatus Liyumba na kuongeza kwamba hata hao viongozi aliowataja katika hati yake ya madai wanavunja Katiba, hivyo wanastahili kuadhibiwa.

“Naiomba Mahakama itoe amri kwamba Mahakama ya Kadhi na OIC hazistahili kuwepo kisheria nchini, hasa Tanganyika,” anadai na kuongeza kwamba Watanzania wanajivunia amani iliyopo nchini na Katiba inayowapa haki sawa kwa wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles