24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mtihani wa ma-DED leo

 Balozi John Kijazi
Balozi John Kijazi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WAKURUGENZI wateule wa halmashauri walioteuliwa na Rais Dk. John Magufuli, leo wanatarajiwa kupewa semina elekezi  na kuapa kiapo cha utumishi wa umma.

Pamoja na hatua hiyo pia wakurugenzi hao wametakiwa kufika na nakala za vyeti vya elimu   na  taaluma.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu  na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, iliwataka wakurugenzi wa halmashauri za majiji, manispaa, miji na wilaya walioteuliwa Julai 7, mwaka huu kufika Ikulu Dar es Salaam wafike na nakala zao halisi za vyeti vya  taaluma (Original Academic Certificates).

“Ieleweke kuwa uhakiki wa vyeti halisi vya taaluma (Original Academic Certificates) unafanywa kwa lengo la kujiridhisha baada ya mchakato wa kawaida wa uhakiki kufanywa kwa kutumia vyeti visivyokuwa halisi (Photocopies).

“Uhakiki huu wa vyeti utaanza saa 2.00 asubuhi na wahusika wote mnaombwa kuingia Ikulu kwa kupitia lango kuu la lililopo upande wa mashariki,” ilieleza taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles