28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mtihani wa kwanza kwa Pau Gasol NBA

Cleveland Cavaliers at Chicago BullsSAN ANTONIO, Marekani

MCHEZAJI wa timu ya mpira wa kikapu ya San Antonio Spurs, Pau Gasol, ameelezwa kuwa atacheza kwa muda nafasi ya katikati ambayo itamfanya kuwa mbali na mshambuliaji mwenzake, LaMarcus Aldridge.

Nyota huyo kwa sasa anatimiza miaka 15 ya kucheza mchezO huo katika Ligi ya NBA nchini Marekani.

Kwa mujibu wa kocha wa timu hiyo, Gregg Popovich, wana mpango wa kutumia aina ya uchezaji wa timu ya Golden State Warriors ambao waliitumia katika michezo ya Western Conference hasa baada ya kumsajili mshindi wa zamani wa tuzo ya MVP Kevin Durant.

Hata hivyo, wakati klabu hiyo ilipomsajili Sant Boi kwa usajili wa miaka miwili akitokea klabu ya Texan Franchise msimu uliopita, alitambua angeziba pengo la mkongwe, Tim Duncan.

Lakini Mhispania, Gasol alitakiwa kubadili nafasi yake kutokana na hasingeweza kucheza nafasi moja na Boi.

Kutokana na ombi hilo kutoka kwa Popovich, Gasol analiona kama mtihani kwake hata hivyo atajaribu kupambana ili kulinda kibarua chake.

Gasol amefanikiwa kubeba ubingwa mara mbili wa NBA akiwa na timu ya Los Angeles Lakers, huku akipitia changamoto nyingi ambazo huenda zimebeba katika mabadiliko hayo.

Nyota huyo aliwahi kucheza mara sita katika michuano ya nyota wa NBA na kuchaguliwa mara nne katika tuzo ya nyota bora wa NBA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles