Mtibwa wapewa mapumziko ya siku nne

0
765

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

BAADA ya kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Kagera Sugar, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila, amewapa mapumziko ya siku nne wachezaji wake kabla ya kuendelea na programu nyingine.

Mtibwa Sugar walikuwa ugenini juzi na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya ndugu zao, Kagera Sugar, mtanange uliochezwa katika Uwanja wa Kaitaba.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katwila alisema mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa lakini walitumia vema uzembe wa wapinzani wao kupata ushindi.

“Tupo njiani (jana) tunarejea nyumbani lakini kwa sasa hatutaendelea na programu yoyote kwani nitawapa mapumziko ya siku nne na baada ya hapo tutaangalia nini kitafuata,” alisema.

Alisema  baada ya kuanza mazoezi ndio atafahamu programu yao itakavyokuwa, ikiwamo kama watacheza mechi za kirafiki au kinyume chake.

Aidha, Katwila, ambaye pia ni kocha wa timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, aliwapongeza wachezaji wake wa Mtibwa kwa kuendelea kujituma na kufanya vizuri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here