20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

MTIBWA SUGAR KUSUKA MIPANGO YA USAJILI DAR

Na THERESIA GASPER,DAR ES SALAAM


 

MABINGWA wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup), timu ya Mtibwa Sugar, inatarajia kupiga kambi jijini Dar es Salaam, huku ikisuka mipango ya usajili kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Timu hiyo ilimaliza nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, baada ya kufikisha pointi 41.

Akizungumza na MTANZANIA jana, kocha mkuu wa timu hiyo, Zuberi Katwila, alisema hadi sasa bado hawajafanya usajili kwa mchezaji yeyote kwani hawana haraka yoyote.

“Tutaweka kambi Dar es Salaam, huku tukiendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao baada ya hapo ndio tutaanza jukumu la usajili katika kikosi chetu kwani hadi sasa bado hatujafanya kwa mchezaji yeyote yule,” alisema.

Alisema bado hawajafahamu wataweka kambi ya muda gani Dar es Salaam kabla ya kurejea Morogoro kuendelea na maandalizi ya ligi.

Akizungumzia kuhusu taarifa za Simba kumhitaji mchezaji wao, Hassan Dilunga, Katwila alisema endapo mabingwa hao wa Tanzania Bara wakimalizana nao hawatamzuia kwani hiyo ni kawaida katika mpira.

“Kila mchezaji ana haki ya kupiga hatua hivyo hata kama ataondoka itawapa nafasi wachezaji wengine ambao walikuwa hawaonekani kucheza na kuonyesha vipaji vyao, mfano kama kina Shiza Kichuya, Mohamed Ibrahim na Salim Mbonde, ambao walikuwa wakichezea katika timu yetu,” alisema.

Mtibwa Sugar huenda inataka kuweka kambi Dar es Salaam kwa ajili ya kuzisoma Simba na Azam ambazo zinashiriki michuano ya Kagame, kabla ya kuanza ligi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,102FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles