Mtibwa Sugar kujipima na KMKM ya Zanzibar

0
542

Theresia Gasper -Dar es salaam

KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila, amesema wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya KMKM ya Zanzibar ili kukiweka fiti kikosi chake kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mtibwa Sugar walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya Burundi na kutoka sare ya mabao 2-2, kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katwila alisema wameshakamilisha usajili wao na sasa anaendelea kuwanoa wachezaji wake ili wawe fiti kabla ya msimu ujao haujaanza.

“KMKM watakuja huku Morogoro, hivyo tunasubiri wakifika tupange tutacheza lini, kwani nahitaji mechi za kirafiki zitakazosaidia wachezaji kuelewana, ukizingatia wengine ni wapya,” alisema.

Alisema wanaendelea na programu ya mazoezi ambapo hadi sasa, hakuna majeruhi, kila mchezaji akionekana kuwa na morali ya hali ya juu.

Katwila alisema anahitaji kuwa na kikosi chenye ushindani Ligi Kuu Bara, ukizingatia kila timu imejipanga vizuri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here