26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mtendaji atakayekwamisha mchakato wa uwekezaji kuchukuliwa hatua

Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mtendaji yeyote atakayekwamisha mchakato w auwekezaji katika eneo lake atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Amesema hayo wakati akijibu maswali ya papo kwa pao kwa Waziri Mkuu, bungeni jijini Dodoma leo ambapo pamoja na mambo mengine amesema serikali kupitia ngazi mbalimbali inaendelea kupokea kero katika wawekezaji.

Amesema uongozi katika ngazi za mikoa na halmashauri wanatakiwa kupokea wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye ngazi hizo na mikoa sasa itawezeshwa kuhakikisha mwekezaji huyo anapata huduma ya uwekezaji na anapata maelekezo sahihi ambapo yako mambo ambayo yanatolewa huko kwenye ngazi hizo.

“Lakini mengine lazima yende Kituo cha Uwekezaji (TIC) na mengine lazima yaende wizarani kwa utekelezaji zaidi kwa hiyo kama yuko mtendaji anakwambia uwekezaji huyo atakuwa hana nia njema na nchi yetu.

“Na popote ambako wananchi mbunge unaona mtendaji tumempa jukumu la uwekezaji anakwambisha mchakato huo hatua kali dhidi yake zitachukuliwa,” amesema.

Aidha, amesema bado serikali inatoa fursa kwa wawekezaji na wamewahusishwa wawekezaji wenyewe pia kumekuwa na vikao na watu mbalimbali rais ambaye amekutana na wafanyabiashara na wawekezaji wengi na watendaji wengine akiwamo yeye wamekutana na makundi hayo mbalimbali kupata kero zinazowagusa wafanyabiashara hao.

“Na sasa hivi tumeandaa mfumo ambayo inaonyesha mabadiliko ya mifumo mbalimbali ya uwekezaji (blue print) ambayo inarahisisha uwekezaji hapa nchini, zaidi na tunaenelea kupokea kero za wawekezaji ili tuendelee kuboresha na ndiyo sababu unaona sasa idadi ya wawekezaji inaongezeka.

“Kwa hiyo niwatoe hofu wawekezaji wote kuja nchini, tuna ardhi, tunazo maliasili, rasimali za kurahisisha uwekezaji huo kama ni viwanda au wakitaka kuchakata madini muhimu ni kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi ili uweze kuwekeza,” amesema Waziri Mkuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles