MTEKETA: NIMEFIKA DARAJA LA MAGUFULI KABLA SIJAFA

0
1344

 

|Mwandishi Wetu, KilomberoMbunge wa zamani wa Kilombero, Abdul Mteketa (CCM), amesema ametimiza azma yake ya kutembelea daraja jipya la Magufuli lililopo wilayani Kilombero mkoani Morogoro.

Akizungumza leo baada ya kutembelea daraja hilo, Mteketa amesema alikuwa ni moja ya viongozi waliopigania ujenzi wa daraja hilo ukamilike haraka wakati Rais John Magufuli alipokuwa Waziri wa Ujenzi katika Serikali ya awamu ya tatu.

“Kama unavyojua katika maisha yangu ya kuumwa pengine nisingeliona hili daraja. Lakini leo nimefika na kuona kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya chini ya Rais Magufuli.

“Watu wa Kilombero, Ulanga na Malinyi tunamshukuru kwa dhati kiongozi wetu mpendwa ambaye amekuwa akifanya kazi kubwa ya kulijenga taifa letu na kuleta maendeleo kwa kasi,” amesema.

Akizungumza hali yake ya kiafya, amesema anamshukuru Rais Magufuli kwani kwa sasa hali yake imeimarika baada ya kupata msaada wa matibabu.

“Awali nilikuwa natembetea kwenye kiti maalumu, lakini kwa sasa ninaweza walau kusimama kwa msaada wa magongo.  Sina la kusema zaidi ya kusema ahsante Rais Magufuli nasi Watanzania tunakuombea kwa Mungu akupe afya njema ili uweze kuongoza taifa letu kwa upendo kama unavyofanya sasa,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here