29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MTAWA KATOLIKI AJIUA KWA KUJIRUSHA GHOROFANI

CLARA MATIMO Na PETER FABIAN, MWANZA


MKURUGENZI wa Fedha na Mipango wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando (BMC), Mtawa Suzan Bartholomew (48), amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya pili ya jengo la hospitali hiyo.

Inaelezwa ni kutokana na   kesi inayomkabili ya kusababisha hospitali upotevu wa Sh milioni 380.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya hospitali hiyo ya Bugando na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna, zilieleza   mtawa huyo aliamua kujirusha  kujitoa uhai kutokana na kukabiliwa na kesi ya upotevu wa   Sh milioni 380.

Kamanda Shanna  alisema Mtawa Suzan aliamua kujiua kwa kujirusha kutoka juu ya ghorofa ya pili ya hospitali hiyo  Agosti 27, mwaka huu   alfajiri lakini alivunjika kiuno na mgongo hivyo kulazwa hospitalini hapo kwa matibabu.

“Baada ya kujirusha alilazwa ICU (Chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum), lakini usiku  wa kuamkia leo (jana) alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu, hivyo mwili wake umehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi  ikiwa ni pamoja na hatua za polisi,” alisema.

Kamanda Shanna alisema siku chache kabla ya kifo chake, mtawa huyo na watumishi wengine wanane wa hospitali hiyo walikamatwa na kuhojiwa kwa tuhuma za ubadhirifu wa  zaidi ya Sh milioni 380 mali ya hospitali hiyo.

“Mpaka sasa tunaweza kusema kifo chake kimetokana na tukio la upotevu wa fedha katika ofisi yake.

“Akiwa kama mkuu wa kitengo cha fedha tulimkamata na kumhoji kwa siku kadhaa kuhusiana na upotevu huo wa fedha na kumuachia kwa dhamana, hivyo wakati akijirusha kujiua alikuwa nje kwa dhamana,” alifafanua.

Habari zaidi kutoka BMC zinadai uongozi wa hospitali hiyo ulianza kufuatilia mapato ya fedha na uliamua kuweka ukaguzi maalumu na kubaini kuwapo  upotevu wa zaidi ya Sh milioni 380 hivyo kuamua kufanyika uchunguzi wa kina.

Baadhi ya wafanyakazi walisimamishwa kazi   kupisha uchunguzi na mtawa huyo akiwa mkuu wa kitengo hicho naye ilibidi akamatwe na kuhojiwa hatua iliyomfanya kuamua kujirusha  kujiua.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles