26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mtatiro: Tutavunja makufuli

MtatiroMGOMBEA ubunge wa   Segerea, Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro amesema atahakikisha wanavunja makufuli yote.

“ Naombeni wananchi tuseme Magufuli…no, in one…kwa miaka yote katika jimbo hili hakuna huduma muhimu ya maji, miundombinu..iwe jua au mvua barabara hazipitiki bado CCM wanataka tuwapeleke Ikulu haiwezekani,”alisema Mtatiro.

Alisema mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli alikuwa wizara inayoshughulika na ujenzi lakini matokeo yake ameshindwa kutengeneza barabara za Segerea sasa anaomba aende Ikulu akafanye nini, apumzike tu!

“Ndugu zangu ilani ya UKAWA ndiyo suluhisho la kero zetu ifikapo Oktoba 25, mwaka huu kura zote wapeni wagombea wa UKAWA,”alisema Mtatiro.

Mtatiro alisema kuna mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Bonna Kalua, amekuwa akipita na mikoba kugawa fedha kwa wananchi.

Alisema  watakachokifanya sasa ni kumvizia na kumpora mkoba huo kisha fedha hizo kugawa kwa vijana na wanawake wanaoteseka kila kukicha.

“Sisi hatuna mashindano ya urembo… tena mwambieni tukiunasa mkoba wake kwa sasa kazi anayo… fedha zote tutagawa kwa wenye shida,”alisema Mtatiro.

TAMBWE HIZA

Naye aliyekuwa Ofisa katika Kitengo cha Propaganda cha CCM, Tambwe Hiza akiwa   katika mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa TP Uzuri,   alieleza kushangazwa kwa kitendo cha Didas Masaburi (aliyekuwa meya wa Dar es Salaam) kugombea ubunge.

“Jambo baya mnalofanyiwa wananchi wa Sinza, Ubungo… yaani wale ambao wamewafanyia mabaya ndiyo wamewaleta kuwa wagombea wenu.

“Eti Masaburi anagombeaubunge muone jinsi watu hawa walivyo na dharau, ”alisema.

Tundu Lissu

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kutoa msimamo wake kuhusu kauli iliyotolewa  na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo kuwa chama hicho hakiko tayari kukabidhi Ikulu kwa upinzani.

Alisema ikiwa Rais Kikwete atakuwa upande wa kiongozi wake, wanachama wa Ukawa kama watakuwa wameshinda Oktoba 25 mwaka huu, watakwenda moja kwa moja   Ikulu kwa nguvu ya umma kudai ushindi wao.

“Katika nchi yetu sheria zetu hazina utaratibu hivyo tunamtaka Jakaya (Rais Kikwete) atwambie ni utaratibu upi atatumia kutukabidhi serikali pamoja na ratiba nzima ya kufanya hivyo.

“Endapo tutashinda halafu wakashindwa kuondoka tutakwenda hadi Ikulu kudai ushindi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles