28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mtandao hatari wa majambazi wanaswa Dar

Simon Sirro
Simon Sirro

Na JONAS MUSHI,DAR ES SALAAM

WATU watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wanadaiwa kukamatwa na polisi wakiwa na zana mbalimbali ambazo hutumiwa na vyombo vya ulinzi zikiwamo silaha za vita na sare za polisi.

Vitu hivyo vinadaiwa kutumiwa na watu hao kufanya   ujambazi.

Inadaiwa kwamba watu hao ni wale waliovamia na kuiba fedha katika jengo la Sophia House lililopo Keko   Dar es Salam wakiwa wamevaa sare za polisi na kutumia gari   ya Noah.

Taarifa zilizolifikia MTANZANIA kutoka chanzo cha kuaminika zilieleza kwamba watu hao ni pamoja na mwanamke mmoja aliyekamatiwa   Bunju  katika Manispaa ya Kinondoni ambako vilikutwa vitu vyote vilivyoporwa na wanaume wawili waliokamatiwa   Mbagala Manispaa ya Temeke,   Dar es Salaam.

Chanzo hicho kilieleza kwamba silaha zilizokamatwa  ni pamoja na bunduki tatu za SMG na risasi zake 260, bastola 16 na risasi zake 526, panga moja na michimbiko mitatu ya kung’olea mageti..

Vitu vingine ni   pingu za chuma 45 na tatu za plastiki, ‘radio call’  12 , kamera ya CCTV moja, gari moja   ya Noah, sare ya polisi jozi moja, ‘pump action tatu na mkasi mmoja.

MTANZANIA lilipomtafuta    Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,   Simon Sirro, kuhusu taarifa hiyo, alisema  taarifa kamili za tukio hilo na kwamba atazitoa leo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles