24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mtaka: Viongozi tutumie nguvu kubwa kujifunza kuliko kuamua

Derick Milton, Simuyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka amewataka viongozi wenzake wenye mamlaka ya kufanya maamuzi katika maeneo ya kazi, watumie nguvu kubwa kujifunza kuliko kufanya maamuzi.

Myaka amesema hayo leo Machi 11, katika mdahalo kuhusu uongozi na maendeleo yenye tija kwa wote ulioendeshwa na taasisi ya Mwalimu Nyerere mjini Bariadi.

Katika mkutano huo wakuu wa wilaya, wakurugenzi na makatibu tawala wilaya zote mkoani humo wameshirikishwa.

Mtaka amesema kiongozi lazima ajifunze kuliko kukimbilia kutoa matamko ambayo haya tija kwa wananchi.

“Viongozi kwa viongozi kugombana ni ujinga na kwangu haliwezi kutokea, wewe Mkuu wa wilaya au mkurugenzi una gari zuri, nyumba, mshahara mzuri, posho nyingi, maji, umeme kwa nini ugombane na mwenzako? Ni ujinga na haufai kuitwa kiongozi” Amesema Mtaka akiwakemea viongozi walio katika ugonvi.

“Tunamsumbua Rais, badala ya kumuacha aongelee mambo ya maendeleo ya nchi tunamfanya aongelee viongozi wanaogombana, anatumia muda wake kusuruhisha watu wanaogombana, hii ni kumdharau Rais, viongozi lazima tuheshimu nafasi za uongozi tulizochaguliwa na Rais wetu Magufuli,” amesema Mtaka.

Mkuu huyo wa mkoa ameongeza kwamba kama viongozi watatumia nguvu walizopewa na Rais kwa kutatua changamoto za wananchi nchi ya Tanzania itakuwa tajiri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles