28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Mtaka awaonya darasa la saba wizi wa mtihani

Derick Milton, Simiyu

Wanafunzi wa darasa la saba nchini, wataanza mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi huku Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akiwaonya wanafunzi hao mkoani humo kujiepusha na vitendo vya wizi wa mtihani huo.

Mtaka ameyasema hayo leo Jumanne Septemba 10, katika Wilaya za Busega na Bariadi alipowatembelea wanafunzi hao kwenye shule mbalimbali ili kujionea maandalizi yao.

Amesema anaamini walimu wamefanya kazi yao vizuri ya kuwafundisha na kuwaandaa wanafunzi hao hivyo ni vema wakafanya mtihani huo wakiwa na ujasiri huku wakipuuza taarifa zozote za kuwepo kwa majibu ya mitihani mahali popote.

“Niwapongeze walimu kwa kazi nzuri waliyoifanya katika kuwafundisha na kuwaandaa kwa kutoa majaribio ya mara kwa mara, kupitia kambi za kitaaluma.

“Niwatahadharishe tu kwamba, msijihusishe na vitendo vya wizi wa mtihani atakayebainika hatua kali dhidi yake zitachukuliwa.

“Mkaufanye mtihani wenu kwa utulivu na ujasiri, asiwadanganye mtu kuwa kuna majibu ya mtihani au mtihani umevuja sehemu fuulani, mkazingatie mlichofundishwa” amesema Mtaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles