31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

Mtaka atunukiwa tuzo ya kiongozi bora aliyeleta mabadiliko kwenye elimu

Derick Milton Simiyu

Taasisi ya Elimu Solution imemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka tuzo ya kiongozi bora aliyefanya mabadiliko kwenye sekta ya elimu na kuongeza ufaulu kupitia kampeni na mawazo yake.

Taasisi hiyo yenye makao makuu yake Jijini Dar es salaam imemkabidhi tuzo hiyo kwenye hafla ya uzinduzi wa kambi ya kitaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne mkoani humo mjini Bariadi jana.

Kabla ya kumkabidhi tuzo hiyo, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Neithan Swed amesema Mtaka aliwashinda viongozi wengine akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo.

Amesema Maka kupitia wazo lake la kuanzisha kambi za kitaaluma kwa wanafunzi wa madarasa ya mitihani ya kitaifa, aliwashinda kutokana na kampeni hiyo kuleta mabadiliko makubwa kwenye elimu mkoani kwake.

“Kupitia kura zilizopigwa na watu mbalimbali, kampeni hii au wazo la mkuu huyu wa mkoa, limeonekana kuwa bora zaidi na limeleta mabadiliko makubwa kwenye elimu, ufaulu umeongezeka, limeshawishi wadau wengi kuchangia elimu na kutambua umuhimu wa elimu,” amesema Swed.

Kwa upande wake Mtaka ameshukuru taasisi hiyo kwa kutambua mchango wa wananchi na viongozi wa Simiyu katika kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles