31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MTAKA AAGIZA UCHUNGUZI FUNZA WANAOHARIBU MAZAO

Na Derick Milton


MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka ameagiza ofisi ya katibu tawala mkoa kutuma wataalamu wa kilimo  kuchunguza funza  wanaodaiwa kuharibu  mahindi   na mtama mkoani humo.

Inaelezwa kuwa funza hao wamesambaa mkoa mzima huku wakiharibu mazao hayo kwa wingi katika wilaya za Busega, Itilima, Bariadi  na Meatu.

Mtaka alitoa agizo hilo kwenye  kikao kamati ya ushauri ya mkoa  baada ya wajumbe wa kikao hicho wakiwamo wenyeviti wa halmashauri kulalamikia uharibufu unaofanywa na wadudu hao.

Wajumbe walisema wadudu hao wamesambaa mkoa mzima hasa katika wilaya za Bariadi  na Itilima.  

Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Joyce Masunga alisema  alipokea malalamiko   kutoka kwa wananchi wilayani  Bariadi waliosema ekari zaidi ya 100 za mahindi zimeharibiwa na funza hao.

“Wananchi wengi baada ya mvua kuanza kunyesha wamefanya kazi kubwa ya kulima mahindi na mtama.

“Tatizo kubwa lililopo kwa sasa ni funza, wamepiga dawa mbalimbali lakini   imeshindikana,” alisema

Wajumbe wengine walisema  wakulima wamejaribu kila dawa    lakini imeshindikana kwa vile  funza hao wameongezeka na kuendelea kuaribu mazao yao.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu ambaye ni mtaalamu wa kilimo, Fabian Manoza alisema   dawa yoyote ya kuua wadudu  itaweza kuangamiza funza hao lakini wajumbe hawakukubaliana naye.

Kwa sababu hiyo, RC  aliagiza wataalamu wa kilimo kutoka ofisi ya mkoa, ofisi za wilaya zote kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti Ukiliguru kwenda katika maeneo husika kuchunguza funza hao na kutafuta dawa sahihi ya   kuwaangamiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles