28.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 25, 2021

MTAENDELEA KUIGA MPAKA LINI?

KUTOJIAMINI ni kati ya tabia mbaya ambazo zinaelezwa kuwa na kiwango kikubwa cha kumkwamisha yeyote kufikia mafanikio ya ndoto zake. Hata kama ukiwa na fedha, lakini ukiwa huamini uwezo wako ni kazi bure tu.

Upo ugonjwa mwingine; uvivu. Hii ni tabia nyingine mbaya inayofananishwa na ugonjwa katika kutafuta ubora wa jambo lako.

Upo uvivu wa namna nyingi, uvivu wa kuchukua hatua na uvivu wa kufikiri. Haya ndiyo matatizo yanayoisumbua sanaa yetu ya Tanzania.

Baadhi ya wasanii, hawataki kujishughulisha. Akili zao wanazipeleka likizo wakiwa na uhakika wa kuiga kazi za wengine.

Hii ndiyo maana leo hii, ukipigwa muziki wa wasanii wa Nigeria na muziki wa Bongo Fleva kwa baadhi ya wasanii, hakuna tofauti. Ukiangalia sinema fulani ya Kibongo unakuta ni kopi na pesti kutoka nchi nyingine.

Wasanii wetu kwa sababu wamependezwa na namna ya uimbaji, uchezaji na staili za Wanigeria, wamejikuta wanaiga.

Huko ndipo tunapoita uvivu wa kufikiri. Wapo wasanii wa Bongo Fleva, ukisikiliza kazi zao utasikia raha namna zilivyo nzuri lakini baada ya muda unagundua kuwa ni copy & paste ya msanii mwingine.

Sanaa yetu itakua lini? Upo ushahidi wa kazi nyingi za kuiga nyingine na kubadilisha lugha. Kuna filamu moja nilikuwa naangalia juzi hapa, yaani imekopiwa kwa wasanii wa Nigeria.

Tatizo nini? Hatuwezi kubuni? Nikisema nielezee upande wa filamu ndiyo kabisa hapafai kwa copy & paste. Yaani  wasanii wetu wanakesha kuangalia kazi za nje ili waone namna gani wanaweza kuiga, badala ya kufikiri na kubuni vyao.

Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba, tunao watu wengi sana hapa Bongo wenye uwezo wa kutunga. Haina maana kwamba kwa sababu wewe ni msanii wa filamu lazima uwe mwandishi wa script.

Siyo kwa sababu wewe ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, basi lazima ujue kutunga. Tumieni vipaji vya watunzi wetu, ambao wapo wengi. Angalia kazi za kampuni ambazo huwatumia watunzi wanavyofanya kazi nzuri.

Hakuna maana kulipua kazi. Tutakuwa tunakwenda mbele hatua moja na kurudi nyingine kumi nyuma. Tuiteje sasa kama siyo upuuzi?  

Wapo baadhi ya wasanii wanaumiza vichwa, wanatumia watunzi kuwatengenezea vitu vizuri, lakini wale wenzangu na miye kazi yao ni kuangalia nani amefanya nini ili aige. Haina maana.

Mnaipeleka wapi sanaa yetu kwa mtindo huu?

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,099FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles