24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mtaalamu wa Lishe aeleza mila zinavyochochea udumavu

Na AVELINE  KITOMARY, DAR ES SALAAM

MKURUGENZI wa Elimu na Mafunzo ya Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Sikitu Kihinga, amesema mila na desturi zinachangi watoto wengi kuwa na lishe duni (udumavu).

Akizungumza katika mafunzo ya waandishi wa habari za Afya  jana jijini Dar es Salaam, alisema asilimia 32 ya watoto wanahali ya udumavu huku Mkoa wa Kagera ukiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto wenye udumavu.

“Nchini Tanzania tatizo la udumavu bado ni kubwa, asilimia 32 ya watoto wamedumaa hii inamaana kati ya watoto 100, watoto 32 wamedumaa, kwa Tanzania tu watoto ambao ni chini ya miaka mitano wako  milioni 9.1 kati ya hao 3.2 wamedumaa hivyo  tatizo ni kubwa. 

“Mkoa unaoongoza kwa udumavu wa watoto ni Njombe kwa asilimia  46.7,  hui ni kwa uande wa kuangalia asilimia lakini mkoa wenye watoto wengi wenye udumavu ni Kagera ukifuatiwa na Kigoma, mikoa kama Kagera inawatoto wengi kwasababu  watu kuzaa sana au mwingiliano wa nchi zingine.

“Katika utafiti wetu tumebaini sababu za udumavu ni mila na desturi, watu wanapenda kula vyakula vya aina moja mfano unakuta watu wanakula tu ugali, wali au ndizi wanasahau vyakula vyingine kama matunda na mboga,”alisema Kihinga.

Alisema sababu zingine ni watoto kutokuangaliwa na wazazi wao badala yake hulelewa na watoto wenzao hali inayosababisha kukosa hata chakula.

“Hii tabia ya kuacha watoto wawalee watoto wenzao ni tatizo, kunamwingine hamlishi mtoto badala yake anakula peke yake na mtoto anakula kidogo, hapo utakuta mama yupo kwenye biashara au shambani anajua mtoto wake analishwa lakini kumbe halishiwi vizuri,” alisema.

Alisema katika mwezi huu wa lishe kwa watoto, wanatarajia kutoa matone ya vitamin A kwa watoto 8,355,900 huku upimaji wa lishe  utafanyika kwa watoto 7,352,645.

“Hapa tunazunguza kuhusu uhamasishaji wa kupekleka watoto kupata matone ya vitamin A, tatizo la vitamin A bado ni kubwa kwa Tanzani, hii imesababisha watoto wasiweze kuona vizuri ndo maana utakuta watoto wadogo wanavaa mewani. 

“Katika huu mwezi wa afya ya mtoto wanaweze kupokelewa kwenye vituo vya afya kupata huduma hii na  inatolewa bure haina madhara yoyote hivyo  watu waachane na imani za kishirikina,”alisisitiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles