27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

MSUVA: NITAENDELEA KASI MOROCCO

Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa timu ya Difaa Al Jadida ya  Morocco, Simon Msuva, amesema kiwango chake kitakua zaidi na atafika mbali pindi Ligi Kuu ya nchi hiyo itakapoanza, Agosti 22, mwaka huu.

Akizungumza na MTANZANIA jana kwa njia ya mtandao, Msuva alisema kwa sasa anaendelea kusoma mazingira ya nchi hiyo na kujifunza vitu mbalimbali kutoka kwa wachezaji wengine wanaotumikia timu hiyo.

Msuva alisema lengo lake ni kuhakikisha anaendeleza kuipatia timu yake mabao kama alivyokuwa akiichezea Yanga ya Tanzania.

“Malengo yangu na hata kasi niliyotoka nayo Yanga itaendelea na huku, kinachotakiwa ni kujifunza vitu taratibu na kuzoea mazingira halisi ili kujipanga kwa ligi,” alisema Msuva.

Alisema mafanikio aliyopata Tanzania kwa kutwaa kiatu cha mfungaji bora mara mbili, yataendelea kuonekana katika klabu yake mpya, kwani ndiyo mipango aliyojiwekea ili kutunza kiwango.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Msuva alifanikiwa kuanza vema katika kikosi chake hicho cha Difaa Al Jadida, baada ya kufunga bao pekee, licha ya timu hiyo kuambulia kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mogreb Atletico Tetuan, kwenye mchezo wa kirafiki.

Msuva, ambaye huchezea pia timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), alisajiliwa na timu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu, aliondoa nchini Julai 26, huku akiwa ameichezea Yanga kwa misimu minne  mfululizo.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles