23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MSUMBIJI YAHITIMISHA KAMPENI YA DHARURA YA CHANJO DHIDI YA KIPINDUPINDU

Wizara ya Afya imekamilisha kampeni ya dharura ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu ambapo hadi sasa wameshafikia watu 745,609 katika wilaya nne zilizokumbwa na kimbunga Idai.

Msemaji wa Shirika la Afya ulimwenguni, WHO mjini Geneva, Uswisi, Tarik Jasarevic amewaambia waandishi wa habari kuwa chanjo hizo zilizotolewa na Mfuko wa chanjo duniani, GAVI zilianza kupatiwa wahusika tarehe 2 mwezi huu na ndani ya saa 24 wahitaji walishafikiwa.

Bwana Jasarevic amesema chanjo zilizosalia zinatumika kuhakikisha kuwa hakuna pengo lolote la wahitaji wanaotakiwa kupatiwa kwenye jamii na pia kwenye maeneo ambayo bado hayajafikiwa.

Kampeni hiyo inayoongozwa na Wizara ya Afya ya Msumbiji, na msaada kutoka WHO, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na Shirika la madaktari wasio na mipaka, MSF, Shirikisho la Msalaba Mwekundu, IFRC na Save the Children, inahusisha wafanyakazi wa kujitolea zaidi ya 1200.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles