28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Msongo wa mawazo chanzo ukosefu nguvu za kiume

Na RAMADHAN HASSAN -DODOMA
SERIKALI imesema sababu za watu kupungukiwa nguvu za kiume ziko nyingi ikiwemo ugonjwa wa kisukari na msongo wa mawazo, huku pia ikikiri kuwa inatambua uwepo wa dawa za kuongeza nguvu hizo zisizo na kemikali ambazo hazijatangazwa rasmi.

Kauli hiyo imetolewa bungeni jana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, aliyekuwa akijibu swali kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Dk. Mwinyi alikuwa akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Ulanga (CCM), Godluck Mlinga.

Katika swali lake, mbunge huyo alitaja orodha ndefu ya dawa za kuongeza nguvu za kiume na kisha kuhoji kama zina madhara kwa watumiaji.

“Kwa sasa kuna wimbi kubwa la dawa za kuongeza nguvu za kiume tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma. Je, ni kwanini kumekuwepo kwa wingi dawa hizo na ni sababu gani ambazo zinapelekea watu wengi kukosa nguvu za kiume?” alihoji Mlinga.

Akijibu, Dk. Mwinyi alisema zipo taarifa nyingi za aina hiyo, lakini jambo jema ni kuongeza uelewa wa wananchi ili kutumia dawa zilizothibitishwa.
Alisema sababu za watu kupungukiwa nguvu za kiume ziko nyingi ikiwemo ugonjwa wa kisukari na msongo wa mawazo, lakini akasema Serikali ilishabaini uwepo wa dawa kwa ajili ya wanaume ambazo hazina kemikali.

Hata hivyo, ameonya matumizi ya dawa ambazo hazijafanyiwa tafiti kwa kuwa si salama kwa matumizi.
Awali, Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo (Chadema) alihoji kama kuna madhara kwa wanaume wanaoongeza maumbile yao pindi wafanyapo mapenzi.

Akijibu, Dk. Mwinyi alisema hadi sasa hana taarifa yoyote ya dawa ambayo inaweza kuongeza ukubwa wa maumbile ya kiume.
Aidha alisema kuwa watu wasitumie dawa yoyote na inatakiwa mtu anayetoa taarifa atoe taarifa ambayo ni ya uhakika.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalumu, Rukia Ahmed Kassim (CUF), alitaka kujua kama Serikali ipo tayari kufungia saluni zote pamoja na kuwachukulia hatua kali wale wote wanaotoa huduma hiyo.
Akijibu hilo, Dk. Mwinyi alisema kuwa yapo madhara mengi ambayo yanatokana na matumizi ya dawa ambazo hazijathibitishwa.

Kuhusu kufunga saluni, Dk. Mwinyi alisema Serikali haioni sababu ya kufanya hivyo bali wizara kupitia TFDA itaendelea kutoa elimu kwa watumiaji pamoja na kuhamasisha watendaji wa afya umuhimu wa kutoa taarifa za ubora na madhara yatokanayo na matumizi ya bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vitenganishi ikiwamo kucha bandia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,455FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles