21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 16, 2022

Msomi UDSM awapa mbinu wanawake 

CHRISTINA GAULUHANGA

-DAR ES SALAAM

WANAWAKE nchini wametakiwa kujitafutia maendeleo kwa kubadili fikra pamoja na kufanya kazi ambazo zilikuwa zinaonekana zinaweza kufanywa na wanaume peke yao.

Akizungumza jana Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Mwanamke ngazi ya Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mkurugenzi wa Taasisi ya Jinsia (UDSM), Dk. Lulu Mahai,  amesema endapo usawa wa kijinsia utasimamiwa na kuzingatiwa ipasavyo unyanyasaji miongoni mwa jamii utatokomezwa.

Alisema tangu kuanza kupewa kipaumbele kwa masuala ya kijinsia miaka ya 90, mabadiliko yameanza kuonekana ambapo kama chuo wanafaya kila jitihada kuondoa unyanyasaji.

“Katika kuzingatia usawa wa kijinsia tunafanikiwa kupata viongozi wa juu wanawake katika elimu ambapo awali ilikuwa ni nadra kumpa madaraka mwanamke,” alisema Dk. Lulu.

Alisema ili kufikia maendeleo na kuondoa unyanyasaji ni lazima wanaume wasiachwe nyuma kwakuwa watachangia kuchochea kufikia malengo.

“Hapa ndio ile dhana ya 50 kwa 50 inapotimia, ni lazima hata hawa wanaume wasiachwe nyuma, ni vyema tukaenda nao ili kuchochea uchumi kukua kwa haraka zaidi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda,” alisema Dk. Lulu.

Alisema chuo hicho kimejikita kuwainua wanawake na tayari wameanza mkakati wa kujenga kituo cha kulelea watoto ambacho kitasaidia kutunza watoto wa wafanyakazi, walimu na wanafunzi ili wasome.

“Wapo wanafunzi wa elimu ya juu ambao tayari wana familia zao na ili kuwaondolea mawazo ya kutunza familia tumejenga kituo kitaanzia ngazi ya awali kwa ajili ya kuwaendeleza kielimu watoto,” alisema.

Dk. Lulu alisema wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wanafunzi wa kike wanaojiunga na elimu ya juu upande wa masomo ya sayansi, hivyo wameamua kutoa kipaumbele kwao ili waweze kupata nafasi nyingi.

Kwa upande wake, mgeni rasmi Balozi wa Norway hapa nchini, Elizabeth Jacobsen, alisema wanawake wakijikita katika shughuli mbalimbali itasaidia kuleta usawa wa kijinsia.

Alisema wakati sasa umefika kwa wanawake kujikita katika shughuli mbalimbali ili kuinua uchumi wa kila mmoja.

Aliipongeza taasisi hiyo kwa kuanzisha kituo cha malezi ya watoto na kusisitiza kitasaidia kuinua elimu hasa kwa wanafunzi ambao wanapata ujauzito wakiwa na umri mdogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,814FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles