24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Msimamo FC kutoka Kata ya Mnyamani yaichapa Karakata FC 3-0

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Timu ya Msimamo FC kutoka Kata ya Mnyamani imeibuka mshindi baada ya kuifunga timu ya Karakata FC kutoka Kata ya Kipawa kwa mabao 3 – 0 katika mashindano ya soka yenye lengo la kuelimisha vijana kujikinga na maambukizi ya VVU (Caflo Vijana Cup).

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la CAFLO, Emmanuel Ngazi, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya soka yenye lengo la kuelimisha vijana kujikinga na maambukizi ya VVU yaliyofanyika uwanja wa Sinai Vingunguti.

Mashindano hayo yanayoendelea katika viwanja vya Sinai Vingunguti yameandaliwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali (CAFLO) ambalo linatekeleza mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU kwa vijana wenye umri wa miaka 14 hadi 25 katika Kata za Vingunguti, Mnyamani, Buguruni, Tabata na Kipawa kwa ufadhili wa GGML.

Mkurugenzi Mtendaji wa CAFLO, Emmanuel Ngazi, amesema timu 16 kutoka katika kata hizo zitashiriki mashindano hayo ambayo yatadumu kwa mwezi mmoja na mshindi atazawadiwa ng’ombe.

“Lengo la mradi ni kuwawezesha vijana kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, waimarishe afya zao ili waweze kushiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo endelevu,” amesema Ngazi.

Amesema kupitia mashindano hayo wanatarajia vijana wengi watapata elimu, mbinu na hamasa ya kujikinga na maambukizi ya VVU, kuimarisha umoja wao katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili na kuongeza kasi ya kujituma na kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo endelevu.

Mratibu Msaidizi wa Kudhibiti Ukimwi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Anselimina Mfinanga, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya soka yenye lengo la kuelimisha vijana kujikinga na maambukizi ya VVU. Kulia ni Mwenyekiti wa CAFLO, Mariam Mlugu na kushoto ni Ofisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Vingunguti, Dominica Balama.

Naye Mratibu Msaidizi wa Kudhibiti Ukimwi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Anselimina Mfinanga, ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo amewataka vijana kuhamasika kutumia michezo kama njia mojawapo ya kujikinga na maambukizi ya VVU.

“Michezo inamjenga mtu kisaikolojia, inamfanya kuwa ‘busy’ na kupanua wigo wa kujishughulisha, kama kijana ni mfanyabiashara atafikiria namna ya kuendeleza biashara yake. Michezo pia ni ajira kupitia mashindano haya wanaweza kupata nafasi ya kuonwa na timu nyingine,” amesema Mfinanga.

Mmoja wa wachezaji wa timu ya Karakata FC, Hashraf Omary, amewashauri vijana wawe na hamasa ya kupima VVU ili watambue afya zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles