29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Msikiti wa Mtambani wateketea kwa moto

Msikiti wa Mtambani ukiwaka moto
Msikiti wa Mtambani ukiwaka moto

Na Mwali Ibrahim, Dar es Salaam

MSIKITI wa Mtambani, uliopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam umeteketea kwa moto.

Moto huo ulianza kuwaka kabla ya sala ya Magharibi katika sehemu ya madarasa ya Shule ya Msingi Mtambani, iliyopo katika majengo ya msikitini huo.

“Moto ulianza kuwaka katika eneo la mabweni ya wanafunzi yaliyopo katika shule hii, lakini kwa bahati nzuri juhudi kubwa zilifanywa ili kuokoa maisha yao.

“Ila kwa bahati mbaya vitu vyote vilivyokuwa kwenye mabweni, hasa ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Muivuno ambao pia huwa wanakuja hapa kujisomea vyote vimeteketea kabisa na hakuna kilichookolewa.

“Mimi nilikuwa ndani ya bweni nasoma, lakini ghafla nilisikia watu wakipiga kelele za moto, nami ndio nikatoka mbio,” alisema Hamis, ambaye ni mwanafunzi wa shule hiyo.

Wanafunzi hao wa shule hiyo walisema tukio la msikiti huo kuwaka moto ni la mara ya tatu kutokea, lakini umekuwa ukidhibitiwa haraka.

MTANZANIA lilipomtafuta Kamanda wa Kipolisi wa Kinondoni, Camilius Wambura, hakupatikana hadi tunakwenda mitamboni.

Msikiti wa Mtambani ni moja ya misikiti maarufu kutokana na kuwa kituo cha wanaharakati wa Kiislamu tangu mwishoni mwa miaka ya 1990.

- Advertisement -

Related Articles

5 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles