MSIGWA AMTAKA DK. KIGWANGALA KUTOA USHAHIDI WA UFISADI WAKE

0
2546

Maregesi Paul, Dodoma

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, atoe ushahidi bungeni juu ya ufosadi wake pamoja na aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Lazaro Nyalandu.

Msigwa amesema hayo bungeni leo Mei 21, alipokuwa akichangia bajeti ya wizara hiyo, kwa mwaka wa fedha 2018/19 iliyowasilishwa na Dk. Kigwangala.

Kwa mujibu wa Msigwa, tuhuma dhidi yake na Nyalandu zilizotolewa na Dk. Kigwangala miezi michache iliyopita haziwezi kufumbiwa macho kwa sababu zilichafua majina yao katika jamii.

“Namuomba Dk. Kigwangala aliekeze bunge amenufaika kiasi gani kupitia kwa mfanyabiashara OBC aliyeko Loliondo kwa kuwa hivi karibuni alionekana akipokea magari kwa ajili ya kukabiliana na majangili,” amesema Kigwangala.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here