29.7 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

MSIGWA ADAI WAFUNGWA SEGEREA WANALALA KWA ‘ALARM’

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), amedai Tanzania kwa sasa kuna msongamano mkubwa wa wafungwa na mahabusu magerezani hususani Gereza la Segerea.

Amesema kutokana na hali hiyo, wafungwa na mahabusu wa gereza hilo wanalazimika kulala upande mmoja mmoja kwa zamu baada ya muda inapigwa ‘alarm’ kisha wanageukia upande mwingine hatua aliyosema ni ukiukwaji wa haki za binadamu na watoto.

Akiuliza swali la nyongeza leo bungeni Msigwa amesema Gereza la Segerea limezidiwa na mahabausu ambapo lina uwezo wa kuchukua mahabusu 700, lakini waliopo sasa ni mahabusu na wafungwa 2,400.

“Ukienda katika magereza zetu kuna msongamano mkubwa sana kwa mfano Gereza la Segerea ambalo nililipitia juzi lina uwezo wa kuchukua mahabusu 700 lakini sasa hivi lina mahabusu na wafungwa 2,400.

“Ni kwanini Serikali imekuwa ikipeleka wanasheria wao ambao wamekuwa wakilazimisha wale ambao wanaweza kupata dhamana waende kukaa mahabusu kama ambavyo kesi zetu zilikuwa zina dhamana lakini mawakili wa Serikali walikuwa wanalazimisha tuende kule tukaongeze msongamano,” amehoji Msigwa.

Akijibu kwa niaba ya Serikali, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha amesema kuwekwa ndani kwa muda mrefu kwa mahabusu si kweli kwamba Serikali haitaki kesi hizo zimalizike haraka.

“Sababu za msingi ni sababu ya usalama wao, wakienda nje wanaweza wakapata matatizo ikiwamo Serikali kuwalinda pili kuna watuhumiwa wakitoka nje wataenda kuharibu ushahidi,” amesema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles