22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

MSICHANA WA CHIBOK AKATAA KURUDI NYUMBANI

ABUJA, NIGERIA

MMOJA wa wasichana wa Chibok waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria ameamua kubakia  na mumewe badala ya kuachiwa huru, kwa mujibu wa msemaji wa Rais wa Nigeria, Garba Shehu.

Msichana huyo, awali alitarajiwa kuwa miongoni mwa kundi la wasichana 82 walioachiwa Jumamosi iliyopita.

Shehu alikiambia kituo kimoja cha habari kuwa wasichana 83 walitarajiwa kuachiwa huru lakini mmoja wao akasema : ‘hapana nafurahi nilipo, nimepata mume.’

Serikali ilikubali kuwaachilia huru wanachama wanne wa Boko haram kubadilishana na uhuru wa wasichana hao, kwa mujibu wa taarifa.

WapIganaji hao wanadaiwa kuwazuilia zaidi ya wasichana 100 kati ya 276 waliowateka katika eneo la Chibok miaka mitatu iliopita.

Kundi hilo pia limewateka maelfu ya raia wakati wa operesheni zao katika eneo hilo huku baadhi yao wakiwa wameozwa wapiganaji na kuzaa nao watoto.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,220FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles