BAADA ya mshiriki kutoka Uganda, Kakunda kujiondoa katika shindano la Maisha Plus East Afrika 2016, mshiriki mpya kutoka Uganda, Ronald Mutebi, ameripoti katika kijiji hicho huku akidai kwamba ana aleji ya ugali.
Kuongezeka kwa mshiriki huyo ambaye alishinda katika usaili wa Uganda lakini alichelewa kupata taarifa ya kufika kijijini, kumeongeza idadi ya washiriki kutoka Uganda kufikia watatu  baada ya mmoja wao kuyaaga mashindano hayo.
Washiriki wengine wanabaki kuwa kama walivyokuwa ambapo Kenya (4), Uganda (3), Burundi (4), Rwanda (4), isipokuwa Tanzania kupungukiwa na mshiriki mmoja kutoka Zanzibar aliyejitoa kutokana na tatizo la ugonjwa, hivyo kubaki washiriki 15.