28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 23, 2021

MSHAURI WA TRUMP ASHINIKIZWA KUJIUZULU

WASHINGTON, MAREKANI


NAIBU Mshauri wa Masuala ya usalama wa Rais wa Marekani, Donald Trump ametakiwa na serikali hiyo ajiuzulu, ikiwa ni miezi mitatu tangu ateuliwe, vyombo vya hapa vimeripoti.

Mshauri huyo, KT Mc Farland, ambaye aliwahi kuhudumu kama mchambuzi wa kituo cha habari cha Fox News ametakiwa kuhudumu kama balozi wa Singapore badala yake, kwa mujibu wa Bloomberg na Reuters.

Hatua hiyo inajiri baada ya Trump kumuondoa Ofisa Mipango, Steve Bannon katika Baraza la Usalama la Taifa (NSC).

Baraza hilo humshauri rais kuhusu masuala ya usalama wa kitaifa pamoja na masuala ya kigeni.

Uteuzi wa Banon mwezi Januari mwaka huu ulizua hofu kwamba suala la washauri wakuu lilikuwa likiingizwa siasa.

Wachambuzi wanasema hatua hiyo ya hivi karibuni inaonyesha kuwa mshauri mpya wa usalama wa Rais Trump, Luteni Jenerali McMaster analifanyia mabadiliko baraza hilo lililoteuliwa na mtangulizi wake.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,900FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles