23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mshahara wa waziri wasimamishwa

 PRETORIA, AFRIKA KUSINI

RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ametoa onyo kali kwa waziri wake wa ulinzi, Nosiviwe Mapisa Nqakula na kusimamisha mshahara wake kwa miezi mitatu kwa kupeleka ujumbe nchini Zimbabwe kwa ndege ya jeshi la anga. Haya ni kwa mujibu wa ofisi ya rais. 

Chama cha upinzani cha Democratic Alliance kilikuwa kimemshutumu Mapisa-Nqakula kwa kutumia vibaya rasilimali za serikali kwa kuruhusu kundi kutoka katika chama tawala cha African National Congress (ANC) kusafiri naye hadi Harare mnamo mwezi Septemba.

Ofisi ya rais ilisema jana kuwa Mapisa-Nqakula alikuwa katika ziara rasmi lakini uamuzi wake wa kuruhusu ujumbe ambao ulikuwa unasafiri kuelekea Zimbabwe kwa shughuli tofauti kuungana naye katika ndege hiyo ulikuwa ‘’kosa la kimaamuzi”. 

 Msemaji wa wizara ya ulinzi hakujibu mara moja maombi ya kutaka maoni kutoka kwa waziri. Mapisa-Nqakula mwenyewe hakujibu mara moja ujumbe uliotumwa kwenye mtandao wake wa LinkedIn. 

Ramaphosa aliahidi kusafisha sifa ya chama cha ANC baada ya miaka 10 ya kashfa chini ya mtangulizi wake Jacob Zuma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles