26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Msekwa: Mchango wa Diaspora unazidi fedha za maendeleo zinazotolewa

Tanzânijas Apvienotâs Republikas ârkârtçjâs un pilnvarotâs vçstnieces Doras Mari Mseèu (Dora Mmari Msechu) tikðanâs ar Latvijas Universitâtes rektoru prof. Mârci Auziòu.NA SARAH MOSSI, STOCKHOLM

KATIKA sehemu ya kwanza ya makala haya iliyochapishwa wiki iliyopita, Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden na katika nchi za NORDIC, Jacob Msekwa, alizungumzia masuala mbalimbali yanayohusiana na mchango wa ubalozi katika kufanya kazi kwa karibu na Watanzania wanaoishi Sweden (Diaspora), wiki hii kiongozi huyo pia anaendelea na mahojiano na mwandishi wetu, SARAH MOSSI, anayefanya ziara katika nchi za NORDIC kukutana na Diaspora katika nchi hizo. Endelea…

 

SWALI: Diaspora wengi wanalalamika wanataka kuja kuwekeza nchini lakini wanakumbana na vipingamizi vingi ikiwamo kutakiwa kutoa rushwa wakidhaniwa kuwa wao wana fedha nyingi na mwisho hukata tamaa, ofisi ya ubalozi mmewahi kukumbana na mtu akilalamikia hali hiyo na mnasaidiaje?

JIBU: Kama nilivyoelez,a jukumu kubwa la ubalozi ni kuwaunganisha Diaspora na mamlaka husika au taasisi husika zilizopo Tanzania na tunatambua malalamiko hayo. Kuna wanaotaka kuwekeza na wapo wanaotafuta misaada kwa ajili ya kusaidia Watanzania wenzao nyumbani lakini wanakumbana na vikwazo hasa pale bandarini au kodi katika kukwamua vifaa vyao.

Sisi ubalozini kila wakati tunajaribu kuwasiliana na makao makuu, kuwaambia wajaribu kuangalia kutafua njia ya kuwasaidia kwa sababu hawa watu wanafanya hivyo kwa mapenzi ya nchi yao.

Na tunawapa moyo juu ya changamoto na matatizo wanaokutana nayo nyumbani na kuwaeleza msivunjike moyo, haya mambo yanaanza kubadilika na somo la Diaspora limeanza kueleweka na kama unavyojua karibuni tu lilifanyika kongamano la Diaspora kule Zanzibar. Na katika kongamano lile, tulijaribu kupigania masilahi ya Diaspora.

Pia tunafanya jitihada za kujaribu kuwaunganisha zaidi, kama vile Denmark wanayo Diaspora yao nzuri sana, Norway pia tunakuja na wazo la kuwaunganisha Diaspora wa nchi zote za Nordic kuweza kufanya kongamano la pamoja kikanda na kujadili matatizo yao na kujaribu kuyasukuma.

SWALI: Ikitokea mmoja wa Diaspora amefariki, ubalozi unasaidia nini katika kuurejesha mwili wa marehemu nyumbani kwa mazishi hususani kwa wale wasiokuwa na uwezo?

JIBU: Kwa upande wetu, tunachoweza kufanya ni kuwa kiungo kati ya ndugu wa marehemu na mamlaka za hapa kuhakikisha tunasafirisha mwili nyumbani. Kuna mwanafunzi alijiua kula Malmo, tulifanya taratibu zote pamoja na kusafirisha mwili nyumbani na hata juzi kulikuwa na Mtanzania amefariki Denmark, tulikuwapo tangu hatua ya mwanzo na tulikuwa na mawasiliano na uongozi wa Diaspora Denmark na mimi mwenyewe nilikwenda kuwakilisha ubalozi katika mazishi. Tuko pamoja katika shughuli zote za Watanzania kama vile harusi, kama nilivyokueleza kwamba Diaspora wanao mchango muhimu.

SWALI: Hii Jumuiya ya Diaspora ya Sweden, mnadhani wamejipanga kweli kupeleka maendeleo nyumbani?

JIBU: Mimi naona wako vizuri na wanajitahidi licha ya changamoto wanazokutana nazo na mifano nimekupa ya mchumi anayejaribu kutusaidia kuandaa semina za kusaidia kuuendeleza uchumi wa nchi za Afrika Mashariki ikiwamo Tanzania.

Kuna wataalamu tunaojaribu kuwaunganisha na wizara mbalimbali katika sekta mbalimbali. Wengine wanataka kwenda kufundisha katika vyuo na wengine wanataka kwenda kutoa uzoefu wao hasa katika sekta ya sayansi na teknolojia.

Na sisi tukigundua kipaji alichonacho Diaspora labda mwanasayansi au fizikia, tunakaa naye na kuongea naye atawezaje kwenda kutoa mchango wake Tanzania ama kwa njia ya kufundisha au kuwekeza licha ya hizo changamoto wanazokutana nazo. Na wanaokutana na changamoto zaidi ni wale wanaotaka kwenda kuwekeza na kama nilivyosema awali kwamba kuna Watazania wa aina mbili.

Moja ni wale kama Watanzania wenye pasipoti za Tanzania bado na wale Watanzania waliochukua uraia wa Sweden na hawa ndio wanaokutana na changamoto zaidi wakienda nyumbani kwa vile sheria zetu mpaka sasa haziruhusu uraia wa nchi mbili, basi huyu atahesabika kama Mswidi na si Mtanzania kwa hiyo akitaka kuwekeza atawekeza kama Mswidi, japokuwa wapo wanaowekeza kimya kimya kwa vile hakuna ufuatiliaji.

Hata tukikutana nao, kikubwa zaidi wanachokizungumza ni suala la uraia pacha na hata Rais Kikwete alipokutana nao na Balozi wetu akikutana nao, swali la msingi wanaloulizia ni la uraia pacha, wengi wangependa suala la uraia pacha liwepo ili liweze kuwasaidia.

Lakini tunajaribu kuwaelezea kama tulivyoona katika Rasimu ya Katiba Mpya kwamba suala la uraia pacha kwa sasa hivi halitakuwapo, lakini mtu yeyote mwenye unasaba na Utanzania atakapokwenda Tanzania atapewa hati ya Ukaazi wa kudumu (Resident Permanent) ambayo itatungiwa sheria ya jinsi itakavyotumika na mipaka yako itatafsiriwa katika sheria ile itakayotungwa. Maoni yanaweza kuwa kwamba mtu anaweza kuwa na haki zote isipokuwa labda kupiga kura.

Hawa wanapata tabu sana katika kuwekeza, hawawezi kwa sababu wanatambulika kama ni Waswidi hawawezi kuwekeza, hawawezi kujenga kwa sababu wanatambuliwa ni Waswidi lakini tunawaeleza hii Resident Permanent itawawezesha kuwekeza na kufanya Maendeleo, hawana tatizo na hilo. Wao wanachotaka ni ule uwezo wa kushiriki katika maendeleo ya nchi yao.

Sisi tunaelewa na hata tukiangalia takwimu za miaka ya hivi karibuni kule nyumbani, utaona kwamba mchango wa Diaspora kwa mwaka ni zaidi ya ile fedha ya maendeleo inayotolewa (Development Corporation).

Hii imeshakuwa approved. Mfano Kenya wanatuma Sh bilioni moja na zaidi kwa mwaka. Kwa hiyo katika kipindi cha miaka mine, mchango wa Diaspora katika kusaidia jamii nchini ni mkubwa kuliko fedha ya maendeleo inayotolewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles