33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

‘Msauzi’ Simba kushusha wakali watatu

Mwamvita Mtanda-Dar es salaam

MKURUGENZI Mtendaji wa Klabu ya Simba ‘CEO’, Senzo Mazingiza amepanga kushusha vifaa vitatu kutoka Afrika Kusinu wakati wa usajili wa dirisha dogo, ambao umepangwa kufunguliwa Desemba 9 mwaka huu na kufikia tamati Januari 16 mwakani.

Mazingiza raia wa Afrika Kusini, amepanga kufanya kazi kubwa ndani ya klabu ya Simba ili kuipeleka kwenye ushindani wa kimataifa.

Kabla ya kutua Simba, Mazingiza alipata kufanya kazi  kwa mafanikio katika klabu kubwa za Afrika Kuisni ambazo ni Orlando Pirates, Sowetto Giants na timu ya Taifa ya nchi hiyo.

Kati ya mikakati aliyonayo bosi huyo ni pamoja na kuwaondoa wachezaji ambao hawana matokeo chanya ndani ya klabu  yake hiyo wakati wa usajili wa dirisha dogo, huku tetesi zikidai straika Mbrazili, Wilker Henrique da Silva anaweza kupigwa panga.

Akizungumza na MTANZANIA jana, chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Wekundu ha ambacho hakikuwa tayari kutajwa jina kilidai kuwa Mazingiza ana mpango wa kuleta wachezaji hao kabla ya Desemba 10 mwaka huu, ambapo wawili watafanya majaribio na mmoja kulamba mkataba moja kwa moja.

 “Mpaka msimu uishe mambo makubwa yatafanyika Simba , huyo CEO anataka maendeleo ya klabu, ndio maana hata alipongudua kocha haeleweki akamtimua haraka.

“Kwanza hao wachezaji wanaokuja nasikia ni hatari, Simba itaunguruma mbona, yaani kabla ya Desemba 10 watakuwa wameshatua,” alisema mtoa habari huyo.

Alisema, kwa sasa kikosi cha simba kina uhitaji wa kuongeza  mabeki wawili, winga pamoja na straika, lakini kwa upande wa mlinda mlango bado wana imani na waliopo akiwemo Aishi Manula.

Chanzo hicho kilieeleza kuwa, tayari Mazingiza amefanya mawasiliano na wachezaji hao, hivyo wakati wowote watatua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles