23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Msanii wa Tanzania kuwania tuzo ya BBC  

Hekima RaymondNA MWANDISHI WETU

MWANAMUZIKI Mtanzania wa muziki wa Classical, Hekima Raymond, ameteuliwa kuwania tuzo za watu wenye ushawishi zaidi kupitia kazi zao.

Tuzo hizo hutolewa na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), Hekima anaungana na watu wengine 49 kufanya kundi la watu 50 wenye ushawishi katika jamii zao kupitia kazi wanazofanya.

Kulingana na tangazo lililotolewa na BBC wiki hii, jopo maalumu litateua washindi watatu watakaopewa tuzo katika hafla maalumu itakayofanyika Julai 4 mwaka huu, huko London nchini Uingereza.

Hekima alisema amefurahi kuteuliwa huko akiamini kwamba hatua hiyo itamwongezea nguvu ya kuendelea zaidi na muziki anaofanya.

Hekima alisema alijifunza mwenyewe upigaji wa piano na uongozaji wa kwaya kwa sasa anajipanga kuufanya muziki wa classic ufahamike zaidi ndani na nje ya Tanzania.

Kupitia kundi lake la Dar Choral Society, Hekima amefanikiwa kuongoza matamasha kadhaa ya muziki wa classic yakiwa yamehudhuriwa na idadi kubwa ya watu wakiwemo mashuhuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles