25.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 20, 2021

Msambazaji sukari atoa uhakika

Yohana Paul -Mwanza

WAKALA wa usambazaji wa sukari,Kampuni ya V.H.SHAH, umetoa uhakika wa upatikanaji wa sukari  kipindi chote cha mfungo wa ramadhani.

Umesema mpaka sasa kuna sukari ya kutosha ghalani ambayo itatosheleza mahitaji ya wananchi.

Akizungumuza na waandishi wa habari  jana, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya V.H.SHAH, Pravin Shah alisema anapokea sukari kutoka viwanda vya uzalishaji vya kama  Kagera, atahakikisha sukari ya kutosha inapatikana na sukari hiyo itauzwa kwa bei elekezi.

Alisema akiwa kama wakala kazi yake, ni kupokea na kusambaza sukari kwa wafanyabiashara kanda ya ziwa,haoni haja ya kuficha  sukari kama ambavyo baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wamedaiwa kufanya,badala yake atatimiza wajibu wake ili kusaidia upatikanaji wa bidhaa hiyo muhimu hasa  katika kipindi hiki cha mfungo wa ramadhani.

“Nawatoa hofu wakazi wote wa kanda ya ziwa, kwani nitajitahidi kuingiza mzigo kulingana na mahitaji,sukari tuliyonayo itauzwa kwa kuendana na bei elekezi iliyotolewa na  niihakikishie serikali kuwa tutaendelea kutoa kushirikiana katika kila hatua ikiwemo katika kipindi hiki cha janga la virusi vya Corona,” alisema Shah.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella aliwataka wakazi wake kutambua  hadi sasa una sukari ya kutosha,amejionea kwa macho yake baada ya kutembelea maghala ya wakala wa sukari, V.H SHAH ambaye anapokea kutoka Kagera Sugar ambao pia wameshapewa kibali cha kuagiza sukari kutoka nchini India.

Alisema  kulingana na uhalisia huo, hategemei kuona mtu yeyote anatengeneza mazingira ya kulangua sukari ili kupandisha bei ya sukari kipindi cha mfungo wa Ramadhani.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,961FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles