25.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Msama awataka wasanii kutumia vema fedha walizokopeshwa na Serikali

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions inayoandaa matamasha mbalimbali ya injili nchini, Alex Msama amewashauri.

Wasanii kutumia mikopo yao waliyopewa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan waitumie katika mambo yaliyokusudiwa ili iweze kuwanufaisha wenyewe katika kuikuza tasnia ya sanaa nchni.

Mikopo hiyo ikiwa ni ya awamu ya pili kwa wasanii Serikali ilitoa Sh milioni 850 kwa wasanii 40 nchini, ambao waliiomba kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Msama ametoa Wito huo leo Februari 12, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa lengo la mikopo hiyo ni kuwasaidia wasanii wote katika kupiga hatia kisanaa.

“Kupitia mikopo hiyo, mfanyie mambo ya msingi, mtunge nyimbo nzuri na mambo mengine ya maendeleo ili mjiinue kiuchumi.

“Tunamshukuru Rais Dk. Samia kwani ana upendo wa hali ya juu, mwenye hofu ya Mungu na mwenye upendo wa dhati kwa Watanzania hasa kwa kuwakumbuka wasanii wote wa Tanzania kwa kuwapa mikopo” amesema Msama.

Aidha, Msama amesema endapo mikopo hiyo ikitumika vizuri itasaidia na wengine kuweza kukopeshwa ili kukuza uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Sambamba na hayo Msama amemshukuru, Waziri wa Utumaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk. Hassan Abbas kwa kufanya kazi nzuri upande wa sanaa ambapo amehimiza wasanii kuunga mkono juhudi hizo za Serikali.

Katika hatua nyingine, Mratibu wa Tamasha la Injili la Pasaka, Emmanuel Mabisa amesema maandalizi ya tamasha hilo maarufu litakalofanyika Aprili 4, mwaka huu jijini Dar es Salaam yapo vizuri.

Amesema wiki ijayo wataanza kutangaza majina ya waimbaji watakaoimba katika tamasha hilo kutoka ndani na nje ya nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,213FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles