24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MSAKO WA MAGARI WAZUA KIZAAZAA PEMBA

Na KHAMIS SHARIF – ZANZIBAR


MSAKO wa magari ya abiria kisiwani Pemba umezua kizaazaa na kuzorotesha huduma ya usafiri kwa wananchi kisiwani hapa.

Kutokana na hali hiyo wananchi wanaotumia usafiri wa umma walilalamikia hatua hiyo kwa kuchelewa kwenda kwenye shughuli zao kwa wakati.

Wakizungumza na MTANZANIA jana kwa nyakati tofauti wananchi hao walisema hawajui sababu ya kuadimika  usafiri huku taarifa zikieleza kwamba ilitokana na ukaguzi maalumu unaofanywa na Bodi ya Mapato Zanzibar.

Akizungumza hali hiyo, Asha Shaibu Haji, alisema  “Tangu saa 12 asubuhi nipo mjini nasubiri usafiri lakini sijaupata na sijui hadi muda wa saa 4.00 asubuhi sijafika ninapoelekea”.

Naye Othman Ali alisema tangu alipotoka Hospitali ya Chachechake asubuhi ameshindwa kupata usafiri wa daladala na kujikuta amekaa kituoni kwa zaidi ya saa tatu bila mafanikio.

Uchunguzi wa MTANZANIA ulibaini kuwa hatua hatua ya ukaguzi uliondeshwa na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZBR) Kanda ya Pemba wa kukamata magari ya abiria yasiyokuwa na vibali ikiwamo bima ilichangia hali hiyo.

Akitoa ufafanuzi kuhusu hali hiyo, Maneja Uwajibikaji na Ushughulikiaji wa Marejesho ya Mapato wa ZRB,  Steven Welema, alisema wameamua kuteke;eza hatua hiyo kwa makusudi kwa lengo la kuwakamata wakwepaji wa bima ambazo hutakiwa kuzitaka kwa mujibu wa sheria.

Alisema hatua ya kutokata bima ni wazi inachangia kuikosesha serikali mapato inayostahili kwa mujibu wa sheria za nchi.

“Tunajua kuna watu wengine wameficha magari yao ndani wakati wa kutekeleza hatua hii, ninachotaka kuwaambia wajue kwamba ZRB ipo na tutaendelea na ukaguzi huu  na wale walioficha magari yao wajue haiwasaidii, sheria itawafikia popote walipo,” alisema Werema

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Shehan Mohamed Shehan, alisema ukaguzi huo ni wa sheria na Jeshi la Polisi linatambua na linafanya kwa kushirikiana na ZRB.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles