22.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

Msajili: Mkapa aliasisi utoaji ruzuku kwa vyama

 CHRISTINA GAULUHANGA -DAR ES SALAAM 

NAIBU Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza amevitaka, vyama vya Siasa nchini kumkumbuka Rais Mstaafu , hatari Benjamin Mkapa katika historia ya Vyama vingi kwakuwa enzi za utawala wake mwaka 1996 alianzisha utoaji ruzuku kwa vyama hivyo. 

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF uliofanyika jana jijini Dar es Salaam, Nyahoza amesema, chama cha CUF nao walikuwa miongoni mwa wanufaika wa ruzuku hiyo kupitia vyama vya siasa vyenye wawakilishi bungeni. 

Alisema wakati wakiendelea na mkutano huo watumie fursa hiyo kumuombea kiongozi huyo ambaye ametangulia mbele ya haki kwakuwa wana historia kubwa naye. 

Akielezea baadhi ya mambo aliyoyafanya ndani ya chama hicho kuwa ni pamoja na mwaka 2001 aliongoza muafaka wa kufanikisha kuleta Umoja wa Kitaifa Visiwani Zanzibar ambao ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa. 

“Mwaka 2005 katika utawala wake alipitisha pia uwepo wa viti maalumu kwa wanawake pia aliongoza, kuendelea na kudumisha siasa za vyama vingi,” alisema Nyahoza. 

Pamoja na hali hiyo alivitaka vyama 19 vya siasa nchini vyenye usajili wa kudumu kuhakikisha katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyia Oktoba 28, mwaka huu wafanye kampeni za kistaarabu, amani na utulivu bila kubughudhi vyama vingine. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,647FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles