23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Msaga Sumu: Mtoto wangu anafuata nyayo zangu

Msaga Sumu
Msaga Sumu

MSANII wa nyimbo za uswahilini maarufu kama Kigodoro, Seleman Jabir ‘Msaga Sumu’, amefurahishwa na tabia ya mwanaye kuonyesha mwelekeo wa kufuata nyayo zake katika uimbaji.

Msaga Sumu aliliambia MTANZANIA kwamba anaamini mtoto wake anafuata nyayo zake kwa kuwa licha ya kuwa na miaka mitano kwa sasa lakini anaimba nyimbo zake zote tena kwa ufasaha.

“Siishi na mwanangu kwa sasa yeye anaishi shule ya kulala ‘boarding’, shule nzuri ya Kiingereza, lakini kila nikienda kumwangalia huwa anapenda kuimba nyimbo zangu nyingi tena anaimba kwa ufasaha kiasi kwamba naamini atakuwa mwimbaji kama mimi.

“Lakini kwa sasa nataka asome kwanza maana yupo shule nzuri ili apate elimu kisha baadaye akifuata nyayo zangu katika uimbaji itakuwa vizuri huku akiwa na elimu yake itamsaidia kujiongoza katika masoko ya muziki wake,’’ alisema Msaga Sumu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles